About

KUZALIWA ni kikundi kabambe cha usanii wa kimataifa, ulioratibiwa kufanyika mnamo mwezi wa kumi (Oktoba), mwaka wa 2016, utakao andaliwa Manchester, UK.

Kampuni ya uigizaji ya The Royal Exchange na Og l esby Charitable Trust, zilizindua mradi unaonuia kuchochea mijadala kuangazia matatizo yasioleta usawa katika huduma za kimatibabu kote duniani.

Waandishi saba shupavu wa kike kote duniani (Kenya, India, Uchina, UK, U.S.A na Brazilia) watalijadili hili swala kwa kina na kuandaa maigizo kuambatana na mtazamo wa nchi zao katika kuzaliwa kwa mtoto .

Mwaka huu wa 2016 Manchester inasherehekea S ayansi ya M ji J kuu wa Uropa. Sherehe ya KUZALIWA inajumuisha matukio ya kiusanii na mijadala ambayo inaunganisha sauti katika ulimwengu wa Sayansi, Sanaa, Kiusomi, Siasa na Misaada.

Mradi huu unatokana na ufanisi mkubwa wa hapo awali ulioletwa na kampuni ya The Royal Exchange, t uzo la uandishi wa michezo ya uigizaji inayojulikana kama The B runtwood P r ize for Playwriting .

The Royal Exchange ndio wakuu wa ukanda kwa maigizo nchini UK mwakwani.

Tovuti hii itafuatilia kazi nyingi za waandishi, watafiti na wanao buni katika kazi zao, kwa hivyo endelea kuandamana nasi ili tukujuze mengi zaidi yalio mapya.

< Back to home